Vijiko na vikombe maalumu vya kupimia mapishi

Ndugu zangu, Naombeni msitumie mugs ama vikombe vya kunywea chai ama vijiko vya kulia chakula kupimia mapishi toka hii tovuti (Taste of Tanzania).

Nimepata maswali machache kwa muda mrefu sasa kuhusu aina ya vijiko na vikombe vya kupimia viungo vya mapishi. Nimeamua kuandika kwa kiswahili kwa sababu wote walioniandikia wengi hawaishi nchi za Ulaya.

Hii ni tafsiri ya vipimo vinavyotumiwa duniani nzima kupimia viungo vya mapishi:

teaspoon(tsp) = kijiko cha chai (kcc)
tablespoon(tbsp) = kijiko cha mezani (kcm)
cup = kikombe (kk)

Mimi vipimo vyangu vyote vya mapishi natumia vikombe maalumu vya kupimia viungo vya mapishi ambavyo kwa kizungu vinajulikana kama Measuring cups (vikombe vya kupimia, na measuring spoons (vijiko vya kupimia).

Hivi ni vyombo amavyo kazi yake ni kupimia vyakula tu. Ni lazima kama unaweza uvinunue. Katika kitabu changu kitakacho fuata tafadhali, tumia hivi vyombo peke yake kupimia viungo vya mapishi.

Mara nyingi vinauzwa vyote kwa pamoja kama set. Utakuta set za vijiko vya chai (tsp = teaspoon) na vijiko vya mezani (tbsp=tablespoon)

Hivi ndo vijiko vyenyewe.

Vijiko vifutavyo ni kutoka www.oxo.com nikipata nafasi nitaweka vijiko vyangu. Unaweza kwenda Amazon kutafuta vingine zaidi vya bei ndogo.

 

vijiko vya kupimia viungo vya mapishi

vijiko vya kupimia mapishi - tsp

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Vikombe vya kupimia viungo vya mapishi

Vikombe vya kupimia viungo vya mapishi - cup

  2 comments for “Vijiko na vikombe maalumu vya kupimia mapishi

  1. naomilukuba
    August 10, 2012 at 4:42 AM

    nipate wapi kitabu chako cha mapishi kwa kiswahili madam miriam kinunda?

    • August 10, 2012 at 8:46 AM

      Kitabu cha pili ndo kitakua kwa lugha zote. Hiki cha kwanza kitakua cha Kiingereza tu.

Comments are closed.