Pilau La Noeli

Pilau la Noeli

Wakati wa Noeli umeisha, lakini kwa sababu wachache wamependelea nitafsiri mapishi yawe kwa Kiswahili. Nimeona ni vizuri nianze na pishi hili maan ni tamu sana. Na pia unaweza kuliandaa wakati wowote wa sherehe yoyote ile. Sasa, kurahisisha mambo, weka makini haya katika viungo

 • kkm – Kikombe / vikombe
 • kjm – Kijiko cha meza / vijiko
 • kjc – Kijiko cha chai / vijiko

Hili ni pilau tamu sana kwa sababu ya mchanganyiko wa korosho, zabibu kavu na zafarani. Wakati wa Noeli ni wakati wa vyakula vitamu vitamu, na mapishi haya ya pilau nimetengeneza kwa sababu hiyo tu. Ili pilau hii iwe inavyotakiwa, lazima utumie zafarani. Kama huna zafarani unaweza kutumia manjano.
Mlo huu ni wakuwatosha watu 6 au 8.

Viungo

 • kjm 2       Pilau masala
 • kkm 1       Mchele
 • mafuta ya kupikia mchele
 • kkm 1/2       vutunguu (viwe vimekatwa vidogo vidogo)
 • jm 1       vitunguu swahumu
 • kjm       tangawizi (iliyotwangwa)
 • kjm 2       pilau masala
 • kkm 1       korosho
 • kkm 1       zabibu kavu (raisins)
 • kjc 1/2       Zafarani (ama kjc 1/4 manjano)
 • kkm 2-3       knorr imechanganywa na maji
 • kkm 1/2       tui zito la nazi
 • kjc 1/2       chumvi ( onja kwanza maana knorr in chumvi)
 • kjm 1       Majani ya Mgiligilani (dhania)

Mapishi

 1. Bandika sufuria, tia mafuta kwenye moto wa kati. Ongeza mchele na vitunguu. Changanya mbaka mchele uwe mweupe na pia unachambuka chambuka.
 2. Ongeza kwenye sufuria vitunguu, tangawizi, na pilau masala. Endelea kuchanganya ili viungo visigande chini ya sufuria pia mbaka vitunguu swaumu viive. Ongeza zafarani.
 3. Kwenye chombo tofauti, changanya tui lamoto na mchuzi wa kuku wa moto
 4. Ongeza mchanganyiko huo wa nazi kwenye sufuria ya mchele ulio jikoni.
 5. Funika sufuria halafu punguza moto uwe kati ya moto wa katikati na wachini. Maji kama yakikauka ongeza korosho, changanya vizuri halafu ongeza nusu kikombe cha mchuzi wa kuku. Onja uone kama chumvi inatosha.
 6. Kama pilau ikikaribia kuiva, ongeza zabibu kavu, majani ya mgiligilani. Changanya vizuri, funika endelea kupika au weka kwenye oveni kama 300F mbaka ukauke vizuri.
 7. Weka mezani wakati bado pilau lina moto.
Chakula hiki ninaenda vizuri na: Kachumbari, na mchuzi wowote ule.

  34 comments for “Pilau La Noeli

 1. joan
  January 27, 2012 at 2:03 AM

  aina ya mapishi inatagemea na mtu mwenyewe.Pishi ni zuri na tamu. Jaribuni. tusikariri mapishi tubadilike wandugu

 2. kemyta
  July 7, 2011 at 11:02 AM

  Habari mwalimu,
  I am sorry but when I follow your instructions to return to the rice option to find this recipe in english… i am only able to find it in swahili. please assist

 3. joyce
  February 9, 2011 at 8:23 PM

  I love this recipe but am not very good in swahili,is it possible to have it in english.

  • February 9, 2011 at 10:42 PM

   I do have this in English. At the top Menu Select Grain – -> then select Rice – -> then you will have different choices of rice recipes, choose Chrismas Menu. Download the pdf. One of the recipes in that pdf file is this pilau recipe in English

 4. November 30, 2010 at 10:00 AM

  Hiyo lazima niambie mke wangu ajaribu kuipika. Asante Bi Miriam.

  • NEEMA
   January 6, 2011 at 6:01 AM

   JAMANI HIYO PILAU NILILIPIKA XMAS ILIYOPITA,NI TAAMU SANA NA MUME WANGU KANISIFIA.ASANTE ENDELEZA MAFUNZO DADA.SIE WENGINE TWAPENDA MAPISHI

   • January 10, 2011 at 6:27 PM

    Asante sana Neema, nashukuru mliipenda. Mimi najaribu kubadolisha mapishi yetu yawe rahisi kupika haraka. Watu wengi wanataka kila mtu apike kama babu zetu walivyokuwa wanapika zamani. Unless Mzungu aje aandike kifupi halafu tumsifu, tukifupisha sisi wenyewe tunajiona tunaaribu mapishi.

 5. zainab mrisho
  November 30, 2010 at 8:13 AM

  kila mtu na mawazo yake.kwa upande wangu mchele mmoja mapishi mbalimbali.mi naona pishi limetulia wadau.

 6. Sara
  November 13, 2010 at 3:46 AM

  mi naona chakula ni kizuri tu
  ahsante mpishi wetu

  wadau, vitunguu swaumu vimewekwa
  ukiangalia maelezo , amesema weka mchele na vitunguu hii ikimaanisha vitunguu maji na vitunguu saumu

  pia pinti ya kusema kwa nini aweke mchele na vitunguu sambamba..
  kwenye maandalizi amesema kata vitunguu vidogovidogo, hii ikiashiria yeye anapendezwa na hali kwamba vitunguu visiive sanaaa ndio raha ya pishi lake
  ni ubunifu tu wandugu
  na ndio raha ya jiko, kuwa mtundu

  ahsante, mi nimejipikia nikajionjea utamu.

 7. rubby
  November 11, 2010 at 12:25 PM

  zafarani ni nini mamie????

 8. Tina
  August 31, 2010 at 5:14 AM

  Naungana na aliyesema mtiririko wa upishi si mzuri, pengine akiweka fresh mtiririko wake ni chakula kizuri pia

 9. Tina
  August 31, 2010 at 5:12 AM

  Wadau someni namba 2, mbona naona kama amesema vitunguu swaumu, pengine alichokosea ni kutaja wakati gani vinawekwa

 10. hidaya
  August 11, 2010 at 11:45 AM

  je pilau hiyo aiwekwi vituguu swaum

 11. Stella Mwakabuta
  July 15, 2010 at 6:02 AM

  Ni kweli pilau gani haihitaji kitunguu swaumu kweli hapo amechemsha kwa siye tunaojua mapishi tunaona hapo amechemsha

 12. layla
  May 30, 2010 at 5:13 AM

  ni kweli mtiririko wa mapishi si mzuri,uliona wapi kitunguu kinawekwa pamoja na mchelle??
  kwa siye tunaojua mapishi tunaona kabissa hapo ni utumbooooooo mtuuupu, SIJAPIKKA BADDOOOO!!!

  • August 8, 2010 at 4:13 PM

   Layla,
   Mapishi yanatofautian kati ya watu na watu, ama nchi na nchi. Katika nchi zote nilizoishi, nimepata bahati ya kujifunza ingalau pishi moja la mchele ambalo pia lina vitunguu kama kiungo kimoja wapo. Sasa inategemea unaishi mji gani Tanzania, lakini najua kuwa mama aliyenifundisha kupika, anapenda sana vitunguu katika wali. Jaribu nahisi utapenda.

 13. Chiku
  May 16, 2010 at 7:04 AM

  Hii pilau ni nzuri..wadau mnajua mapishi hata kama ya kitanzania mara nyingi ni tofauti kidogo na hutegemea unatoka kona gani ya TZ. Maana pwani wanapika hivi na Arusha wanapika hivi..so cha msingi ni kupenda kujifunza mambo mapya..na kama kitu haupendi basi ignore it wengine watakipenda it is as easy as that..

 14. Chiku
  May 16, 2010 at 7:03 AM

  Hii pilau ni nzuri..wadau manajua mapishi hata kama ya kitanzania mara nyingi ni tofauti kidogo na hutegemea unatoka kona gani ya TZ. Maana pwani wanapika hivi na Arusha wanapika hivi..so cha msingi ni kupenda kujifunza mambo mapya..na kama kitu haupendi basi ignore it wengine watakipenda it is as easy as that..

 15. getrude deogratius
  April 28, 2010 at 4:00 AM

  mm nahitaji kujua mapishi ya aina mbalimbali

 16. Mimi
  March 14, 2010 at 9:23 PM

  MImi ninafikiri Knorr ni Chicken Broth( Supu ya kuku inayotokana na kuchemshwa nyama ya kuku) halafu pia hii aina ya Pilau ni nzuri kwa kweli sielewi unasema mtiririko waupishi sio mzuri yaani una maana gani.

  • August 8, 2010 at 4:16 PM

   WaTanzania wengine wanaita “Kidonge cha supu”. Asante Mimi

  • August 8, 2010 at 4:17 PM

   WaTanzania wengine wanaita Kidonge cha supu. Asante Mimi

 17. mpishi 1
  February 8, 2010 at 1:17 PM

  Mpishi yoyote anayepika sana na anejua kupika, anajua knorr ni nini. zinapatikana madukani jijini Dar. Sijui huko nje, lakini mimi huwa nanunua mtaani kwetu.

 18. mpishi
  February 4, 2010 at 7:28 PM

  Knor ndo nini kwa ufupi pilau ya ainahiyo si nzuri pili mtiririko waupishi si mzuri

Comments are closed.