Pilau La Noeli

Friday, January 22, 2010
By Miriam Rose Kinunda

Pilau la Noeli

Wakati wa Noeli umeisha, lakini kwa sababu wachache wamependelea nitafsiri mapishi yawe kwa Kiswahili. Nimeona ni vizuri nianze na pishi hili maan ni tamu sana. Na pia unaweza kuliandaa wakati wowote wa sherehe yoyote ile. Sasa, kurahisisha mambo, weka makini haya katika viungo

  • kkm – Kikombe / vikombe
  • kjm – Kijiko cha meza / vijiko
  • kjc – Kijiko cha chai / vijiko

Hili ni pilau tamu sana kwa sababu ya mchanganyiko wa korosho, zabibu kavu na zafarani. Wakati wa Noeli ni wakati wa vyakula vitamu vitamu, na mapishi haya ya pilau nimetengeneza kwa sababu hiyo tu. Ili pilau hii iwe inavyotakiwa, lazima utumie zafarani. Kama huna zafarani unaweza kutumia manjano.
Mlo huu ni wakuwatosha watu 6 au 8.

Viungo

  • kjm 2       Pilau masala
  • kkm 1       Mchele
  • mafuta ya kupikia mchele
  • kkm 1/2       vutunguu (viwe vimekatwa vidogo vidogo)
  • jm 1       vitunguu swahumu
  • kjm       tangawizi (iliyotwangwa)
  • kjm 2       pilau masala
  • kkm 1       korosho
  • kkm 1       zabibu kavu (raisins)
  • kjc 1/2       Zafarani (ama kjc 1/4 manjano)
  • kkm 2-3       knorr imechanganywa na maji
  • kkm 1/2       tui zito la nazi
  • kjc 1/2       chumvi ( onja kwanza maana knorr in chumvi)
  • kjm 1       Majani ya Mgiligilani (dhania)

Mapishi

  1. Bandika sufuria, tia mafuta kwenye moto wa kati. Ongeza mchele na vitunguu. Changanya mbaka mchele uwe mweupe na pia unachambuka chambuka.
  2. Ongeza kwenye sufuria vitunguu, tangawizi, na pilau masala. Endelea kuchanganya ili viungo visigande chini ya sufuria pia mbaka vitunguu swaumu viive. Ongeza zafarani.
  3. Kwenye chombo tofauti, changanya tui lamoto na mchuzi wa kuku wa moto
  4. Ongeza mchanganyiko huo wa nazi kwenye sufuria ya mchele ulio jikoni.
  5. Funika sufuria halafu punguza moto uwe kati ya moto wa katikati na wachini. Maji kama yakikauka ongeza korosho, changanya vizuri halafu ongeza nusu kikombe cha mchuzi wa kuku. Onja uone kama chumvi inatosha.
  6. Kama pilau ikikaribia kuiva, ongeza zabibu kavu, majani ya mgiligilani. Changanya vizuri, funika endelea kupika au weka kwenye oveni kama 300F mbaka ukauke vizuri.
  7. Weka mezani wakati bado pilau lina moto.
Chakula hiki ninaenda vizuri na: Kachumbari, na mchuzi wowote ule.

Tags: , ,

15 Responses to “Pilau La Noeli”

  1. mpishi

    Knor ndo nini kwa ufupi pilau ya ainahiyo si nzuri pili mtiririko waupishi si mzuri

    #255
  2. mpishi 1

    Mpishi yoyote anayepika sana na anejua kupika, anajua knorr ni nini. zinapatikana madukani jijini Dar. Sijui huko nje, lakini mimi huwa nanunua mtaani kwetu.

    #257
  3. Mimi

    MImi ninafikiri Knorr ni Chicken Broth( Supu ya kuku inayotokana na kuchemshwa nyama ya kuku) halafu pia hii aina ya Pilau ni nzuri kwa kweli sielewi unasema mtiririko waupishi sio mzuri yaani una maana gani.

    #281
  4. getrude deogratius

    mm nahitaji kujua mapishi ya aina mbalimbali

    #309
  5. Chiku

    Hii pilau ni nzuri..wadau manajua mapishi hata kama ya kitanzania mara nyingi ni tofauti kidogo na hutegemea unatoka kona gani ya TZ. Maana pwani wanapika hivi na Arusha wanapika hivi..so cha msingi ni kupenda kujifunza mambo mapya..na kama kitu haupendi basi ignore it wengine watakipenda it is as easy as that..

    #330
  6. Chiku

    Hii pilau ni nzuri..wadau mnajua mapishi hata kama ya kitanzania mara nyingi ni tofauti kidogo na hutegemea unatoka kona gani ya TZ. Maana pwani wanapika hivi na Arusha wanapika hivi..so cha msingi ni kupenda kujifunza mambo mapya..na kama kitu haupendi basi ignore it wengine watakipenda it is as easy as that..

    #331
  7. layla

    ni kweli mtiririko wa mapishi si mzuri,uliona wapi kitunguu kinawekwa pamoja na mchelle??
    kwa siye tunaojua mapishi tunaona kabissa hapo ni utumbooooooo mtuuupu, SIJAPIKKA BADDOOOO!!!

    #355
  8. Stella Mwakabuta

    Ni kweli pilau gani haihitaji kitunguu swaumu kweli hapo amechemsha kwa siye tunaojua mapishi tunaona hapo amechemsha

    #424
  9. Layla,
    Mapishi yanatofautian kati ya watu na watu, ama nchi na nchi. Katika nchi zote nilizoishi, nimepata bahati ya kujifunza ingalau pishi moja la mchele ambalo pia lina vitunguu kama kiungo kimoja wapo. Sasa inategemea unaishi mji gani Tanzania, lakini najua kuwa mama aliyenifundisha kupika, anapenda sana vitunguu katika wali. Jaribu nahisi utapenda.

    #500
  10. WaTanzania wengine wanaita “Kidonge cha supu”. Asante Mimi

    #501
  11. WaTanzania wengine wanaita Kidonge cha supu. Asante Mimi

    #502
  12. Mpishi
    Knor pia watu waita Kidonge cha supu.

    #503
  13. hidaya

    je pilau hiyo aiwekwi vituguu swaum

    #514
  14. Tina

    Wadau someni namba 2, mbona naona kama amesema vitunguu swaumu, pengine alichokosea ni kutaja wakati gani vinawekwa

    #593
  15. Tina

    Naungana na aliyesema mtiririko wa upishi si mzuri, pengine akiweka fresh mtiririko wake ni chakula kizuri pia

    #594

Leave a Reply

Search Recipes

Subscribe

Archives

Categories